Mahakama yaitupilia mbali kesi ya kuzaa na mke wa mtu iliyokuwa ikimkabili Josephat Mwingira
Dkt. William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba
mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha kujua vinasaba
vya mtoto (DNA).
Dkt. Morris ambaye ni mume wa (mdaiwa wa pili, Phills Nyimbi) aliiomba mahakama itoe amri ya mkewe, Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA ili aweze kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.
Alidai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa huyo wa kiume.
Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, amesema Dkt. Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonyesha mahusiano ya kimapenzi kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.
Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa Morris ni matokeo ya mahusiano ya kimapenzi kati ya Phills na Mchungaji Mwingira.

No comments