Kamanda wa Polisi Arusha apata ajali mbaya ya gari
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amepata ajali mbaya ya
gari katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada ya gari alilokuwa
akitumia kusafiria kupasuka gurudumu ‘tairi’ ya nyuma na kupoteza
muelekeo.
Kamanda Mkumbo amepelekwa katika hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha kwa ajili ya matibabu zaidi huku ikielezwa kuwa ameumia vibaya maeneo ya kichwani.
Chanzo:NIPASHE
Gari aliyokuwa amepanda Kamanda Charles Mkumbo
Taarifa hizo zilizothibitishwa na mlinzi wa Kamanda Mkumbo kwa njia
ya simu ya RPC, amesema Mkumbo amepata ajali hiyo ambapo ndani ya gari
aliyokuwa akiitumia walikua watu watatu akiwemo msaidizi wake pamoja na
dereva.Kamanda Mkumbo amepelekwa katika hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha kwa ajili ya matibabu zaidi huku ikielezwa kuwa ameumia vibaya maeneo ya kichwani.
Chanzo:NIPASHE


No comments