Breaking News

Wimbo mpya wa Alikiba wakumbwa na majanga YouTube

Wimbo wa Alikiba unaokwenda kwa jina la Mvumo wa Radi ambao umetoka Mei 11 mwaka huu, umekumbwa na tatizo kufuatia idadi ya watazamaji (views) kuto kuongezeka licha ya kuwa ni wimbo unaotazamwa zaidi katika mtandao wa YouTube kwa sasa. Wimbo huo ambao hadi jana Jumamosi tayari ulikuwa na watazamani 690,000, hadi sasa katika mtandao wa YouTube unaonesha umetazwa mara 783,000 jambo ambalo linaonesha kuwa kuna tatizo kwani idadi imeongezeka taratibu sana ikilinganishwa na watu wanaotazama video hiyo. Kufuatia tatizo hilo, Alikiba amesema kuwa anafahamu jambo hili na kwamba amewasiliana na Makao Makuu ya YouTube Afrika ili waweze kurekebisha suala hilo. “Tunafahamu tatizo la kutokuongezeka kwa views kwenye akaunti ya YouTube ya ALIKIBA, na tupo kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na makao makuu ya YouTube Africa ambao wanafanya kila jitihada kutatua tatizo hili kwa haraka iwezekanavyo” ameandika Alikiba. Aidha, amewataka mashabiki wake na watu wote kuendelea kuwa wavumilivu wakati wakitafuta suluhisho la tatizo hilo, huku akiwasihi kuendelea kutazama video hiyo. “Shukrani kwa uvumilivu wenu na support mnayoendelea kutupa! Endeleeni kuangalia video ya #MvumoWaRadi.”

No comments