Mbunge Ashauri Wanaume Kuoa Wake Wengi
Mbunge mmoja nchini Kenya ameibua hoja kuwataka wanaume kuoa wanawake wengi, ili kuweza kusaidia malezi ya familia na kupunguza watoto wa mitaani.
Mbunge huyo anayejulikana kwa jina la Gathoni wa Muchomba kutoka kaunti ya Kiambu, amesema ameona ni vyema iwapo wanaume wataoa wanawake wengi kwani watoto wengi nchini humo wamekuwa wakilelewa na mzazi mmoja, jambo ambalo linasababisha malezi mabaya na watoto kuangukia kwenye matatizo.
“Nimetoa haya matamshi kama kiongozi wa Kiambu kwa sababu ya matatizo ambayo tunayo ya watoto kulelewa na ‘single mother’, nadhani hilo linaweza likawa suluhisho litasaidia kwenye malezi ya familia, kama uko na uwezo wa kutunza na kutumikia kwa mahitaji yake yote, naona tumekuwa tunaacha yale ambayo tulikuwa tunafuatilia miaka iliyopita”, amesema Mbunge huyo.
Mbunge huyo amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.
Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.
No comments