Breaking News

Kauli hii yamponza Manara, Kichuya ni Lionel Messi “La Pulga” asisitiza kadri wanavyo umia atazidi kuwachoma

Baada ya msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara kumfananisha mshambuliaji wake, Shiza Ramadhi Kichuya na mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi kwa staili ya uchezaji wao hii ikiwa imefuatiwa baada ya hapo jana kuisaidia Taifa Stars kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 0.Manara amewajibu wale wote waliyokuwa wakimpinga kauli hiyo kwa kuandika kuwa watu hawapendi kuona akiwasifia wachezaji wake na kusisitiza atafanya hivyo kwakuwa ni moja ya wajibu wake. Kuna watu wachache waliojua Soka Instagram wanatamani nife eti kwa kuwa nnasifia sana wachezaji wangu..nawaambia sitaacha kwa kuwa hii ni moja ya wajibu wangu..kama vile nnavyowasifia wa timu nyingine wanapofanya vema au kama nyie mlivyowwsifu walioshushwa na Mungu..kadri mnavyoumia mm nnazidi kuwachoma..halaf guys why muhangaike na hii page?hata kama mm maarufu sio kihivyo..c mwende kwa msemaji wenu jomoni…au kule miyeyusho, Na wallah msipokuja kulike na kucomment nahama nchi

No comments